Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 29, 2022 Local time: 10:29

Boko Haram wajikusanya katika ngome yao ya Gwoza


Wapiganaji wa Boko Haram wakipita katika mji wa Chibok katika jimbo la Borno Nov. 9, 2014.

Ripoti kutoka Nigeria zinasema wapiganaji wa kundi la wanamgambo wa Boko haram wanakusanyika kwenye ngome yao ya Gwoza na kuimarisha nguvu zao kutoka maeneo mengine.

Chanzo kimoja cha kijasusi ambacho kinaangalia hali ilivyo kimeiambia Sauti ya Amerika-VOA kwamba vikosi vya jeshi vinakaribia kwenye mji na wanamgambo huwenda wanajiandaa kuulinda mji wa Gwoza, ambao ni moja ya miji mikubwa ya mwisho wanayoidhibiti huko kaskazini-mashariki mwa Nigeria.

Chanzo hicho kinasema vikosi vya kundi la Boko haram vinasafiri kuelekea Gwoza kutoka kwenye makambi yao ya kisiasa yaliyo karibu na msitu wa sambisa. Gwoza inapatikana kiasi cha kilomita 135 kusini ya mji mkuu wa Borno, Maiduguri.

XS
SM
MD
LG