Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 14:10

Afrika Mashariki yaimarisha ushirikano wa biashara na Marekani


Sherehe za kutia saini mkataba wa biashara kati ya Marekani na Afrika Mashariki mjini Washington

Marekani imetia saini mkataba wa bishara na mataifa matano ya Jumuia ya Afrika Mashariki mjini Washington siku ya Alhamisi katika lengo la kupunguza vizuizi vya biashara na kutoa msaada wa kiufundi kuimarisha usafirishaji wa bidhaa za kilimo za Afrika Mashariki kwa masoko ya Marekani.

Mawaziri wa biashara na uwekezaji wa Kenya, Tanzani, Uganda, Rwanda na Burundi, walitia saini mkataba unaokamilisha juhudi zilizoanzishwa mwaka 2012, za kuimarisha biashara kati ya pande hizi mbili.

please wait
Embed

No media source currently available

0:00 0:02:54 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Mwakilishi wa biashara wa Marekani Michael Froman aliueleza mkataba huo kuwa ni "hatua muhimu ya kuongeza kile ambacho tayari kimedhihirisha kuwa ni ushirika wa matumaini na yenye nguvu"

"Mkataba huu unakabiliana na masuala matatu muhimu ya ushirikiano wa kuondowa vizuizi vinavyokwamisha biasjara, kwanza inaimarisha ushirikiano katika masuala ya forodha,pamoja na utekelezaji wa makubaliano wa shirika la biashara duniani WTO."

Anasema kuwepo na mkataba huo utapunguza sana masharti na vikwazo vya biashara vya pande mbili. Utaimarisha ushirikiano wa kuwaelimisha waatalamu wa Afrika Mashariki juu ya usalama wa chakula na mifugo, ili kuwezesha bidhaa za kilimo na mifugo kuweza kusafirishwa katika masoko ya Marekani. Na hatimae mkataba huo unawezesha kuwepo na ushirikiano wa kiufundi kusawazisha sheria na maeguzi ya bishara na kuweka viwago vya pamoja vya biashara.

Bw Froman anasema, hivi sasa biashara kati ya Marekani na nchi hizo zitakuwa chini ya usimamizi wa Jumuia ya Afrika Mashariki bila ya kuwa nahaja ya kuwa na mikataba ya biashara na kila nchi kati ya hizo tano

Hata hivyo Waziri wa Afrika Mashariki kutoka Tanzania Harrison Mwakyembe anasema mkataba huu unaimarisha hivi sasa juhudi za kuunda soko la pamoja la Afrika ya Mashariki

"Mkataba huu unafuatia mafanikio yaliyopatikana katika juhudi za mungano wa mataifa yetu tangu 2005, kunganisha pamoja bishara zetu na kuojndowa matatizo ya forodha na kubuni mazingira ya kuvutia uwekezaji wa ndani na nje."

Waziri wa biashara na uwekezaji wa Tanzania Abdallah Kigoda anasema makubaliano haya yanazipatia nchi za Afrika Mashariki kuimarisha mifumbo na viwango vyao vya biashara kuweza kupeleka bidhaa zaidi za kilimo Marekani.

Wachambuzi wa biashara wanachukulia mkataba huo kama hatua muhimu na kubwa katika kuelekea makubaliano ya biashara huru kati ya bara la afrika na marekani. Kufuatana na idara ya biashara ya marekani biashara kati ya mataifa ya afrika mashariki na marekani imefikia jumla ya dola bilioni 2.8 hapo mwaka jana ikionfgezeka kwa asili mia 103. Marekani imeagizia bidhaa zilizofikia jumla ya dola milioni 743 wakati marekani imesafirisha jumla ya bidhaa zake kufikia dola bilioni 2.0. wachambuzi wa nasema hivi sasa marekani inajaribu kwa kasi kuifikia china ambayo ndio mshirika mkuu wa biashara na afrika ikifuatiwa na umoja wa ulaya.

XS
SM
MD
LG