Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 00:34

“Jihad John” hatimaye atambuliwa.


Wapiganaji wa Islamic State huko Aleppo January 6, 2014.
Wapiganaji wa Islamic State huko Aleppo January 6, 2014.

Taarifa za vyombo vya habari zinasema mwanamgmbo wa kundi la Islamic State aliyegubika uso wake na ambaye mara kwa mara ameonekana katika video kadhaa akiwakata vichwa mateka hatimaye ametambuliwa, ingawa vyanzo vya habari vya usalama vinaonya kwamba taarifa hizo huenda zisiwe sahihi.

Ripoti zinakariri marafiki wa Mohamed Emwazi wakisema wanaamini ndiye kijana mrefu mwenye lafudhi ya Kiingereza anayeonekeana kwenye video za Islamic State na kupewa jina la “Jihadi John.”

Vyanzo viwili vya serikali ya Marekani vinaamini Emwazi ndiye mtu huyo aliyegubika uso wake. Msemaji wa baarza la usalama wa kitafa la Marekani anasema maujai ya raia wa Marekani na kundi hilo la Islamic State yanaendelea kufuatiliwa kwa karibu. Mwanamume huyo wameonekana kwa video kadhaa akiwa amevalia mavazi meusi, na kugubika uso wake . Emwazi anaripotiwa kuwa Muislam mzaliwa Kuwait, ambaye ni mkaazi wa London.

XS
SM
MD
LG