Wamiliki wa mashirika makuu ya vyombo vya habari nchini Kenya MOA, wanasema wanataka muda zaidi ili kuweza kujitayarisha vilivyo kuhamisha matangazo kutoka mfumo wa analog kuelekea dijital.
Hatua hiyo inafuatia kuzimwa kwa mfumo wa analog na Halmashauri ya Mawasiliano Kenya CAK mwishoni mwa wiki na kusababisha vituo vikuu vya televisheni vya Citizen, Nation TV, KTN na Q-TV kufunga matangazo yao kote Kenya.
Mwenykiti wa MOA Sam Shollei anasema “hatukupata muda wakutosha, kwa sababu tulipata liseni tuliyokua tukiomba kwa miaka mitatu mine hivi, tuliipata tarehe 25 Novemba. Halafu muda mfupi baadae CAK ikatangaza kwamba itafunga mfumo wa analog tarehe 31 mewzi Disemba. Mwezi moja baadae. Tumesema muda huo hautoshi.”
Bw. Shollei anasema mbali na muda kuna tatizo la kulazimishwa kutumia kampuni mbili za kupeperusha matangazo yao ile ya Signet ya Shirika la matangazo la Kenya KBC na kampuni ya kichina. Anasema mashirika ya kibinafsi yanahitaji jukwa lao pia la kuweza kupeperusha matangazo yao.
Kwa upande wao chama cha Waandishi Habari Kenya KUJ kimetowa wito kwa serikali na wadau wa vyombo vya habari kutanzua mvutanohuo wao juu ya kuhamisha mfumo wa analog kuelekea dijitali kwa haraka iwezekanavyo
KUJ inadai kwamba bila ya kutanzuliwa mzozo huo kwa haraka wafanyakazi wengi wa vyombo vya habari watapoteza kazi zao na mafanikio makubwa yaliyopatikana ya uhuru wa vyombo vya habari Kenya yatakuwa hatarini.
Mwenyekiti wa KUJ, Oscar Obonyo anasema utata mkubwa uliyopo ni kwamba wadau wote wa vyombo vya habari hawakushirikishwa vilivyo katika utaratibu wa kubadili mfumo wa matangazo ya televisheni kutoka analog kuelekea dijital.
Anasema kilichotokea ni kwamba mashtaka ya mahakamani yaliyochukua muda yamesababisha mashirika ya matangazo kutokuwa na muda wakujitayarisha ili kuhamisha matangazo yao kuelekea dijitali.
Kwa wakati huu mashirika mawili ya KBC na K24 ndizo zinatangaza kwa dijitala huko Kenya lakini kutokana na kwamba wateja hawajapata vifaa vya kupoka matangazo ya dijitali isipokua wachache tu basi Wa-Kenya wengi hawapati matangazo ya televisheni tangu siku ya Jumamosi.
Chama cha Waandishi wa Habari Kenya kinatowa wito kwa serikali na wadau wote wa vyombo habari kutanzua kwa haraka mvutano huo kabala ya kusababisha athari kubwa kwa uhuru wa matangazo nchini mwao.