Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Machi 26, 2023 Local time: 06:34

Polisi 6 wa Tanzania wajeruhiwa katika shambulio la Tanga


Mapango ya Amboni wilaya ya Tanga nchini Tanzania

Kamishna wa operesheni na mafunzo wa Jeshi la polisi la Tanzania Paul Changonja anasema askari 6 waloshiriki katika operesheni ya kuwasaka majambazi walokua wamejificha katika mapango ya Amboni wilaya ya Tanga wamejeruhiwa na wanatibiwa hospitalini.

Mahojiano na Kamishna Chagonja wa Tanzania
please wait

No media source currently available

0:00 0:04:18 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Akizungumza na Sauti ya Amerika siku ya Jumamosi, Kamishna Changonja anasema kikosi cha pamoja cha usalama kilipelekwa katika eneo la mapango ya Amboni baada ya kupata habari za kuaminika kwamba silaha zao zilizoibwa mwezi wa Januari zimefichwa huko.

Amasema kufika huko majambazi walkifanya shambulio la kushtukiza na kusababisha majeraha hayo na waliweza kukimbia kutoka njia iliyokuwa wazi upande wa juu ya mapango, lakini anaamini kuwa baadhi yao walojeruhiwa baada ya mapigano makali wakati wa alfajiri siku ya Jumamosi.

Katika taarifa aliyotowa, Kamishna Changonja ametowa wito kwa watu kuripoti ikiwa wanamuona mtu yeyote aliyejeruhiwa katika jamii yao.

XS
SM
MD
LG