Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 25, 2024 Local time: 15:43

Vuruga zakumba bunge la Afrika Kusini.


Kiongozi wa chama cha upinzani cha Economic Freedom Fighters (EFF) Julius Malema, akiwasili bungeni na vazi la kuonyesha kuwaunga mkono wachimba makaa ya mawe huko Cape Town, Afrika Kusini, May 21, 2014.
Kiongozi wa chama cha upinzani cha Economic Freedom Fighters (EFF) Julius Malema, akiwasili bungeni na vazi la kuonyesha kuwaunga mkono wachimba makaa ya mawe huko Cape Town, Afrika Kusini, May 21, 2014.

Bunge la Afrika Kusini lilkumbwa na vurugu Alhamisi wakati wabunge wa upinzani walipomzuia rais Jacob Zuma kutoa hotuba yake ya mwaka juu ya hali ya kitaifa.

Maafisa wa usalama waliingia bungeni na kuwaondoa kwa nguvu wabunge wa upinzani kutoka chama cha Economc Freedom Fighters (EFF) ikiwa ni pamoja na kiongozi wao Julius Malema ambaye aliingilia kati hotuba ya rais akiuliza ni lini Bw.Zuma atalipa zaidi ya dola milioni 20 fedha za umma zilizotumika katika kukarabati nyumba yake binafsi.

Baada ya kuondolewa kwa wabunge wa chama cha Bw.Malema, wabunge kutoka chama kikuu cha upinzani Democratic Alliance walipinga hatua ya kuwafukuza wenzao bungeni na kuondoka kwenye bunge hilo.

Bw.Zuma hata hivyo aliamua kuendelea na hotuba yake huku akishangiliwa na wabunge wa chama chake cha ANC, akielezea mafanikio waliyopata tangu kumalizika kwa utawala wa wachache miongo miwili iliyopita.

XS
SM
MD
LG