Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 17:11

Putin afanya ziara ya siku mbili Misri.


Picha za rais wa Russia Vladimir Putin katika maeneo ya daraja la Qasr El Nile huko Cairo, Misri, Jumatatu, Feb. 9, 2015.
Picha za rais wa Russia Vladimir Putin katika maeneo ya daraja la Qasr El Nile huko Cairo, Misri, Jumatatu, Feb. 9, 2015.

Rais wa Russia Vladmir Putin aliwasili Misri jana kwa ziara ya siku mbili inayolenga kuinua mahusiano ya Moscow na Cairo.

Bw.Putin alilakiwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Cairo Jumatatu na rais wa Misri Abdel Fattah Al –Sissi.

Kiongozi huyo wa Russia ni kiongozi muhimu asiye wa kiarabu kumuunga mkono rais Sissi ambaye anakumbana na ukosoaji mkali kutoka Washingon wa kuwakandamiza wapinzani tangu kiongozi wa zamani Mohamed Morsi kung’olewa madarakani wakati akiwa mkuu wa majeshi Julai 2013.

XS
SM
MD
LG