Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 02, 2022 Local time: 10:23

Tunisia na DRC zafuzu nusu fainali


Timu za Tunisia na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, zimefuzu kucheza hatua za robo fainali za michuano ya Mataifa ya Afrika, yanayo endelea nchini Equatorial Guinea.

Kutoka katika kundi B, timu hizo zimefanikiwa kufuzu baada ya kutoka sare ya goli moja kwa moja, huku timu nyingine za kundi hilo za Cape Verde na Zambia zikiaga mashindano hayo rasmi.

Tunisia inaongoza kundi hilo kwa kufikisha pointi 5, huku DRC ikiwa na pointi 3 sawa na Cape Verde, lakini DRC inafuzu kutokana na tofauti ya magoli.

Zambia, mabingwa wa zamani wa michuano hiyo wanaondoka katika michuano hiyo wakishika mkia katika msimamo wa kundi hilo.

XS
SM
MD
LG