Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 07, 2022 Local time: 10:12

Mrembo Paulina Vega wa Colombia ashinda taji la Miss Universe.


Miss Colombia Paulina Vega akivikwa taji lake la Miss Universe huko Miami, Jumapili, Jan. 25, 2015.

Mrembo Paulina Vega wa Colombia amevikwa taji la Miss Universe baada ya ushindani mkali Jumapili katika mji wa Miami , jimbo la Florida Marekani.

Bi Vega mwenye umri wa miaka 22 alimshinda Nia Sanchez wa Marekani aliyechukua nafasi ya pili na Diana Harkusha kutoka Ukraine alishika nafasi ya tatu.

Jumla ya washindani 88 walishiriki katika shindano hilo, ambalo linashirikisha wanawake kati ya umri wa miaka 18 hadi 27 ambao hawajaolewa na hawana wototo.

XS
SM
MD
LG