Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 21, 2023 Local time: 08:32

Kitandawili katika CAN 2015 ni nani anaondoka nani anabaki


Mchawi wa timu ya DRC kwnye mchuano dhidi ya Cape Verde Ebebiyin

Wafuatiliaji na mashabiki wote wa kandanda Afrika na duniani kote kwa ujumla wajiuliza, jee ni nani atasonga mbele katika robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrioka 2015 huku Equatorial Guinea?

Hakuna atakae weza kujibu suala hilo hadi baada ya kuanza na kumalizika kwa awamu ya tatu ya michuano ya kundi siku ya Jumamosi hadi Jumanne.

Kwa mara ya kwanza katika michuano ya finali za Kombe la Mataifa Afrika imekuwa vigumu kusema nani anasonga mbele katika robo finakli kutokana na matokeo ya awamu ya kwanza mabpo takriban makundi yote timu zimekwenda sare isipokua kundi la C, kundi la kifo.

Katika kundi hilo, Senegal, Ghana na Algeria kila moja alipata ushindi mara moja lakini Senegal inaongoza ikiwa na point 4 na Ghana na Algeria kila moja point 3, Afrika Kusini inaondoka patupu lakini inaweza kuharibu hali ya mambo ikipata ushindi katika mchuano wake wa mwisho na Ghana.

Katika kundi D kila timu, Ivory Coast, Cameroon, Guinea na Mali kila mmoja ana pointi 2.

Kaika kundi A wenyeji Equatorial Guinea wanahitaji kushinda leo kuweza kupata nafasi ya kusonga mbele dhidi ya Gabon, ambayo inapointi 3 na wenyeji pointi 2. Congo inaongoza ikwa na pointi 4, huku Burkina Faso inapointi 1.

Na katika kundi la B Tunisia inaongoza ikiwa na pointi 4 na timu nyingine zote Zambia Cape Verde na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kila mmoja pointi 1.

Basi ukiangalia namna mambo yalivyo ni kufa na kupona katika awamu ya mwisho inayoanza Jumapili.

XS
SM
MD
LG