Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 04, 2024 Local time: 01:42

Tanzania: Profesa Muhongo ajiuzulu.


Profesa Sospeter Muhongo, waziri wa zamani wa nishati na madini Tanzania
Profesa Sospeter Muhongo, waziri wa zamani wa nishati na madini Tanzania

Aliyekuwa waziri wa nishati na madini nchini Tanzania Profesa Sospeter Muhongo amemwandikia Rais Jakaya Kikwete barua ya kujizulu rasmi kufuatia sakata la Tegeta Escrow lililotikisa nchi kwa muda mrefu.

Vyombo vya habari nchini Tanzania vimemnukuu Profesa Muhongo akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake akisema kuwa yeye ni mtu msafi na hajahusika katika kadhia hiyo ya rushwa ya uchotaji wa mabilioni ya fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow.

Alisema ameamua kujizulu bila kupata shinikizo akiona kwamba yeye ndio atakayemaliza mjadala huo wa sakata ya rushwa ya Tegeta Escrow.

Ameahidi kuzungumza na watanzania hivi karibuni ili kuwaeleza undani na ukweli wa akaunti ya Tegeta Escrow.

XS
SM
MD
LG