Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 23:48

Uchaguzi wa rais DRC huenda ukacheleweshwa.


Rais wa DRC Joseph Kabila akiwa mkutanoni huko Kampala Uganda.
Rais wa DRC Joseph Kabila akiwa mkutanoni huko Kampala Uganda.

Afisa mmoja wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo anasema uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika 2016 unaweza kucheleweshwa kwa mwaka mmoja.

Msemaji wa Serikali Lambert Mende aliiambia Radio France International Ijumaa kwamba uchaguzi unaweza kufanyika 2016 au 2017.

Vyama vya upinzani vimemshtumu rais Joseph Kabila kwa kujaribu kuongeza muda wake kupitia mapendekezo ya sheria ambayo yatahitaji kukamilisha kwa sensa ya watu ya kitaifa kabla ya uchaguzi kufanyika.

Mswada ulipata uungaji mkono hapo katika bunge wiki hii lakini Jumatatu upinzani ukatoa mwito wa maandamano na kuvamia majengo ya bunge kuzuia mswada huo kupita.

Bw.Kabila hivi sasa anahudumu katika muhula wake wa pili wa kipindi cha miaka mitano na katiba inamzuia kugombania urais kwa muhula wa tatu.

XS
SM
MD
LG