Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 09:08

Papa Francis ahimiza amani Sri Lanka.


Papa Francis akizungumza katika hekalu la Buddha. Asia
Papa Francis akizungumza katika hekalu la Buddha. Asia

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis ameendelea kuhimiza ujumbe wa umoja kwa Sri Lanka kwenye misa iliyohudhuriwa na maelfu ya watu katika mji mku wa nchi hiyo.

Umati mkubwa ulimiminika kwenye barabara karibu na ufuo wa bahari mjini Colombo siku ya jana kumshangilia Baba mtakatifu akiwa amebebwa na gari lake maalum. Wakati wa misa hiyo , alimtawaza mchungaji Joseph Vaz akisema kuwa utawazo huo ambao ni wa kwanza nchini Sri Lanka unaashiria umuhimu wa kuwa na amani inayopita migawanyiko ya kidini.

Vaz alikuwa mmishonari wa karne ya 17 anayekumbukwa kwa kuifufua imani ya kikatoliki wakati waumini walikua wakiteswa na wareno wenye imani tofauti. Kesho Alhamisi Baba Francis ataelekea Ufilipino kwa ziara ya juma nzima ya eneo hilo.

XS
SM
MD
LG