Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 17:29

Kikwete amvua uwaziri Tibaijuka.


Rais Kikwete akihutubia wazee wa Daresalaam.
Rais Kikwete akihutubia wazee wa Daresalaam.

Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania amemvua madaraka ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi Anna Tibaijuka kufuatia shutuma za kupokea fedha katika njia zilizo kinyume na maadili katika kashfa ya fedha inayojulikana kama Tegeta Escrow.

Akizungumza mjini Dar es salaam Jumatatu Rais Kikwete alisema mashauriano yanaendelea kuhusiana na mawaziri na maafisa wengine wa wizara za serikali ambao walitajwa katika kashfa hiyo. Hao ni pamoja na Waziri wa Nishati na Madini Sospita Muhongo na katibu wake mkuu Eliakim Maswi.

Waziri Tibaijuka ambaye aliwahi kuongoza taasisi ya Umoja wa Mataifa – HABITAT – alitajwa kupokea zaidi ya shillingi bilioni moja na nusu kutoka kwa mfanyabiashara, James Rugemalira, aliyekuwa na hisa katika kampuni ya IPTL.

Bibi Tibaijuka amekuwa akijitetea kuwa fedha hizo ziliingizwa kwenye akaunti yake kwa ajili ya kuendeleza shule binafsi anayoendesha, lakini katika maelezo yake Rais Kikwete alisema kuwa waziri huyo hakuweza kumpa rais maelezo ya kuridhisha kwa nini fedha hizo ziliingia kwenye akaunti yake binafsi

XS
SM
MD
LG