Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 04, 2024 Local time: 00:35

Marekani yasikitishwa na sheria mpya ya ugaidi Kenya.


Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Jen Psaki akizungumza na waandishi wa habari.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Jen Psaki akizungumza na waandishi wa habari.

Serikali ya Marekani imesema pamoja na kuunga mkono mapambano dhidi ya al-Shabab nchini Kenya, imesikitishwa na sheria mpya ya ugaidi nchini humo ambayo haikuwapa muda wa kutosha raia kuijadili na hasa vipengele vinavyozuia uhuru wa vyombo vya habari na wa kukusanyika na kuwanyima hifadhi wakimbizi .

Pia imeitaka serikali ya Kenya ihakikishe kwamba juhudi zake za kupambana na ugaidi zinaheshimu haki za watu wake na kufuata katiba ya nchi na utawala wa sheria.

Nalo kundi la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch pia limeeleza masikitiko yake kwa kupitishwa kwa sharia hizo mpya, na kuongeza kuwa huenda zikatumiwa vibaya vya vyombo vya usalama nchini Kenya.

XS
SM
MD
LG