Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 31, 2023 Local time: 19:20

Bunge la Kenya lapitisha mswada wa kuimarisha usalam


Kundi dogo la waandamanaji wakilalamika dhidi ya sheri a mpya ya usalama waloweza kuwapenya na kuwapita polisi walokuwa wanazuia maanadmano.

Wabunge wa Kenya waliweza kupitisha mswada mpya wenye utata, juu ya usalama baada ya kupigana magumi bungeni siku ya Jumatano, katika kikao maalum kilichokuwa na mabishano makali.​

Mungano unaotawala wa Jubilee umekuwa ukihimiza kupitishwa kwa mswada huo kama njia ya kuiwezesha taifa hilo kukabiliana na ongezeko la kitisho cha ugaidi.

Mbunge Muthoni Wahome anasema, "wakenya wanahamu ya kuimarisha usalama, kwa sababu wametaabika sana kama nchi, hatutalegeza kamba. Kama wanajubilee na watu wenye nia njema tutapitisha mswada leo."

Wabunge wa upinzani wanabisha kwamba vipengele vya mswada huo utawapokonya waananchi haki zao msingi waloweza kujinyakulia baada ya kupitishwa kwa katiba mpya, na kudai hawakupata muda wa kutosha kuujadili mswada.

Alfred Keter mbunge mwengine anasema, "ninataka kuona baraza la wawakilishi lililoungana ili tuweza kupitisha mswada mzuri zaidi. Na haijalazimu kuharakisha mambo, hatuna haja ya kumaliza sasa, hii si mwisho wa dunia, tumewapoteza Wakenya wengi na tunataka sharia za kudumu. Hebu tupeane muda.

Mbunge mmoja asiyetaka kutajwa anasema mswada ulopitishwa umefanyiwa marekebisho muhimu na hauko sawa na ule ulopendekezwa.

Mabalozi wa mataifa 9 nchini Kenya akiwemo balozi wa Marekani, walitoa taarifa Jumatano kueleza wasi wasi wao kuhusiana na mswada huo. Wanasema wanaunga mkono mipango ya kuimarisha usalama lakini sio kwa kuvuruga haki za binadam.

Kabla ya kikako cha asubuhi cha bunge, usalama uliimarishwa katika njia zote za Nairobi na kuna watu walokamatwa walipojaribu kuandamana kupinga kupitishwa kwa mswada huo.

XS
SM
MD
LG