Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 10:24

Obama atangaza mabadiliko ya kihistoria katika uhusiano na Cuba


Alan na Judy Gross wakiwasili Washington kwa mkutano na waandishi habari, Dec. 17, 2014.

Rais Barack Obama ametangaza mabadiliko makubwa ya kihistoria katika sera ya Marekani kuelekea Cuba na ameanza kuondowa vikwazo vya nusu karne na taifa hilo la kikomunisti.

Hatua hiyo imetangazwa kuwa ni enzi mpya katika ushirikiano kati ya Marekani na Cuba ambao ulivunjwa tangu mkomunisti Fidel Castro kuchukua madaraka katika taifa hilo la kisiwa mwaka 1959.

Fidel Castro na wenzake 1959
Fidel Castro na wenzake 1959

Uhusiano ulizorota baada ya serikali ya Castro kuanza kutaifisha mali za Marekani na kuanza mlolongo wa ukiukaji wa haki za binadam iliyoipelekea Washington kuiwekea vikwazo.

Akizungumza Jumatano Rais Obama amesema "nimemwambia waziri wa mambo ya nchi za nje John Kerry kuanza mara moja majadiliano na Cuba ili kuanzisha tena uhusiano wa kidiplomasia ambao tuliuvunja tangu Januari 1961."

Mabadiliko aliyoyatangaza ni pamoja na kufunguliwa upya ubalozi wa Marekani mjini Havana, baada ya karibu nusu karne. Marekani ina mpango pia wa kupunguza masharti ya biashara, shughuli za benki na usafiri wa Wamarekani hadi kisiwa hicho, ambacho wakati mmoja kilikuwa kivutio kikubwa cha mapumziko kwa Wamarekani.

Rais Obama amesema hatua yake ya Jumatano inafuatia wito wa kibinafsi kutoka kwa Papa Francis. Lakini kilichochochea mabadiliko haya yote ni tangazo la Cuba kumachilia huru Alan Gross, Mmarekani aliyekuwa anafanya kazi na Idara ya Maendeleo ya Kiamtaifa ya Marekani, USAID, aliyekuwa kizuizini Cuba kwa miaka mitano.

XS
SM
MD
LG