Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 29, 2022 Local time: 21:48

Jengo la gorofa tano laanguka Nairobi Kenya.


Jengo la ghorofa tano limeanguka katika mji mkuu wa kenya, Nairobi Jumatano alfajiri na kusababisha kifo cha mtu mmoja na inasadikiwa takriban familia 30 zimekwama kwenye vifusi vya jengo hilo.

Kwa mujibu wa mwandishi wetu wa Nairobi, jengo hilo lipo katika eneo la kaloleni karibu na uwanja wa michezo wa city stadium. Juhudi za uokozi zinaendelea kufanyika ili kuwaokoa watu waliokwama ndani ya vifusi.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation jengo hilo ambalo lilikuwa linaendelea kujengwa lilikuwa na wakazi ambao walikuwa wakiishi katika ghorofa ya chini, ya kwanza na ya pili wakati ghorofa nyingine tatu za juu zikiwa zinaendelea kujengwa.

XS
SM
MD
LG