Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 15, 2024 Local time: 06:21

Mtu mwenye silaha Sydney aendelea kushikilia mateka.


Mateka mmojawapo akikimbilia polisi nje ya mgahawa wa Lindt ambako mateka wengine bado wanashikiliwa huko Sydney, Australia, Des. 15, 2014.
Mateka mmojawapo akikimbilia polisi nje ya mgahawa wa Lindt ambako mateka wengine bado wanashikiliwa huko Sydney, Australia, Des. 15, 2014.

Mzozo wa utekaji nyara huko syden, Australia unaendelea saa kadhaa baada kuanza mapema hivi Jumatatu. Watu watano wamekimbia kutoka kwenye mgahawa uliopo Sydney katika wilaya ya biashara ambako mtu aliyekuwa na bunduki amekuwa akiwashikilia mateka watu kadhaa.

Inakadiriwa takriban kuwa watu kumi mpaka 25 bado wanashikiliwa. Habari za televisheni kutoka kwenye eneo hilo zimemuonyesha mfanyakazi wa Lindt Chocolate Café na wateja wawili wakikimbia kuwapita polisi ambao wameuzunguka mgahawa huo na kuliziba eneo hilo.

Baadaye watu wengine wawili walitoka mbio kutoka kwenye jengo hilo. Ofisi za karibu ziliondolewa wafanyakazi kama hatua ya tahadhari. Mateka wameonekana wakiwa wamesimama na mikono yao juu ikiwa imeegemezwa kwenye madirisha.

XS
SM
MD
LG