Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 21, 2025 Local time: 23:05

Wafanyakazi wa Bunge Weusi Marekani wajiunga na maandamano.


Picha ya jengo la bunge la Marekani
Picha ya jengo la bunge la Marekani

Zaidi ya wafanyakazi wa bunge mia moja weusi katika bunge la Marekani walitoka nje bunge hilo Alhamisi kupinga maamuzi ya mabaraza ya mahakama katika miji wa New York City na Ferguson , Missouri ambako hakuna hukumu iliyotolewa kwa maafisa polisi wazungu waliohusika katika vifo vya wanaume weusi wa Marekani ambao hawakuwa na silaha katika kipindi cha mapukutiko.

Kundi la wafanyakazi wa bunge, wengi wao wakiwa Wamarekani weusi takriban 150 walikusanyika kwenye ngazi za jengo la bunge muda mfupi baada ya saa tisa na nusu alasiri konyesha mshikamano wao na waandamanaji , katika kile kiongozi wa dini bungeni Barry Black alichosema ni ‘Sauti ya wale wasiosikika’.

Bwana Black alisema; “ Leo hii wakati watu kote katika taifa hili wanaandamana kutetea haki katika ardhi yetu , tusameheni pale tuliposhindwa kupaza sauti zetu kwa wale ambao hawakuweza kuzungumza au kupumua wenyewe,” aliomba.

Alitoa mwito Wamarekani wasisahau historia ya nchi yao, akisema waliostahili kuchukua hatua wameshindwa na kuomba Mungu awafariji wale wanaoomboleza ambao wanajua uchungu wa kupoteza wapendwa wao.

Wabunge hao waliongeza sauti zao katika maandamano kote nchini wiki iliyopita baada ya maamuzi ya majopo ya majai walioteuliwa na mahakama kupinga hukumu kwa Daniel Pantaleo polisi mzungu wa New York aliyehusika na mauaji ya Julai 17 ya Eric Garner alipokuwa akifanya kazi yake kama mchuuzi wa katika eneo la Staten Island.

Garner alikabiliwa na maafisa kadhaa wa polisi huku Pantaleo akimkaba koo, na kusikika kwenye ukanda wa video akisema “I cant’ Breath” (Siwezi Kupumua) kabla ya kupoteza maisha yake.

XS
SM
MD
LG