Mwanaharakati wa elimu Malala Yousfzai na mwenzake wa kutetea haki za watoto kutoka India Kailash Satyarthi Jumatano wameandika historia wakikabidhiwa tuzo ya Amani ya ulimwengu mjini Oslo, Norway.
Malala ambaye ana umri wa miaka 17 ndiye mdogo sana kuwahi kupokea tuzo hiyo huku Satyathri akiwa mzaliwa wa kwanza wa India kupata tuzo hiyo. Wote wawili watagawana tuzo hiyo ya dola million1.1 na pamoja na kutoa hotuba kwenye hafla hiyo. Kabla ya sherehe kuanza, Malala aliwapa barua viongozi wa dunia akiwasihi waufanye mwaka wa 2015 kuwa salama na wenye haki kwa watoto.
Alisema kwamba ingawaje tuzo hii inaonyesha kwamba vizazi vinaweza kuitisha maisha mema kwa watoto ni lazima pia kuwa na hatua za kufanya kila mtoto akawa na uhakika wa maisha ya usoni.