Baraza la Maaskofu wa Burundi limetowa wito kwa seikali ya Bujumbura kuitikia wito unaotolewa na vyama vya upinzani na asasi za kiraia kuhusiana na matayarisho ya uchaguzi mkuu wa 2015.
Siku ya Jumapili Asasi za Kiraia zimeitaka Tume ya Uchaguzi ya Taifa CENI kusitisha zowezi la kuwaandikisha wapigaji kura, zikieleza kwamba vitambulisho vya bandia vinatumiwa kuwaandikisha watu.
Mwandishi wa habari Haidallah Hakizimana anasema, mwezi uliyopita vyama vya upinzani vilowa wito kama huo kidai kuwepo na kasoro zitakazo hujumu utaratibu kamili wa uchaguzi. lakini waziri wa ndani alisema hizo ni kasoro chache ambazo haziwezi kuharibu utaratibu mzima wa uchaguzi.
Wakati huo huo upinzani unavutana na mungano wa vyama vinavyotawala taifa hilo la Afrika ya Kati juu ya ikiwa Rais Pierre Nkurunziza anaweza kugombania kiti chake kwa mhula wa tatu wakati katiba inaeleza mtu anaweza kubaki mihula miwili pekee katika uwongozi.