Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 04, 2024 Local time: 01:24

Anti-Balaka wasema wataunda chama cha kisiasa.


Wapiganaji wa Anti-balaka huko Jamhuri ya Afrika ya kati , Agosti. 28, 2014.
Wapiganaji wa Anti-balaka huko Jamhuri ya Afrika ya kati , Agosti. 28, 2014.

Wanamgambo wa Kikristo katika Jamhuri ya Afrika ya Kati wanasema wataweka silaha chini na kuwa chama cha kisiasa.

Afisa wa juu wa kundi la wanamgambo la anti-Balaka alitangaza Jumamosi usiku kwamba kuanzia sasa wanamgambo hao watapambana tu kupitia mbinu za kisiasa.

Anasema mwanachama yeyote ambaye atafanya shambulizi atafikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Kundi hilo linasema vugu vugu lao litaitwa jina jipya la Central African Party for Unity And Development.

Jamhuri ya Afrika ya Kati imekumbwa na ghasia tangu waasi wa kiislam waitwao Seleka kutimua serikali ya rais Francois Bozize madarakani, wakisema serikali yake ilikuwa inawakandamiza waislam kaskazini mashariki.

Ukiukwaji wa haki za binadamu uliofanywa na kundi la Seleka, ulipelekea kuibuka kwa waasi wa wa Kikristo waitwao anti-Balaka, waliofanya vitendo vya ukatili kwa misingi ya kidini na kusababisha mamia ya waislam kutoroka nchini humo.

XS
SM
MD
LG