Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 16:56

Obama asema vita dhidi ya Ebola vitachukua muda mrefu.


Rais Barack Obama, katika mkutano na timu yake ya usalama w ataifa pamoja na ya afya ya umma akipewa taarifa kuhusu mapambano na Ebola, huko White house. Nov. 18, 2014.
Rais Barack Obama, katika mkutano na timu yake ya usalama w ataifa pamoja na ya afya ya umma akipewa taarifa kuhusu mapambano na Ebola, huko White house. Nov. 18, 2014.

Rais wa Marekani Barack Obama anasema vita dhidi ya Ebola bado vina safari ndefu kushindwa licha ya mafanikio ya kuwatibu watu waliopimwa na ugonjwa huo hapa Marekani.

Alizungumza Jumanne huko White house baada ya mkutano na timu yake ya kupambana na Ebola. Bw.Obama alisema kuendelea kwa mlipuko wa ugonjwa huo barani Afrika kunaonyesha ni jinsi gani ilivyo muhimu kuendeleza vita dhidi ya ugonjwa huo.

Amesema hadi pale mlipuko utakapomalizwa Afrika magharibi, bado kutakuwa na hatari kwa kiasi fulani kwa watu wengine duniani kuambukizwa.

Hiyo hiyo Jumanne wajumbe wa bunge la Marekani walitathmini hali ya waafrika magharibi wanaojaribu kukabiLiana na mlipuko huo wa Ebola, kwa kuzingatia mahitaji yao ya dawa, uchukuzi na kuelimisha watu juu ya ugonjwa huo.

XS
SM
MD
LG