Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 17:56

NATO yaisihi Russia kurudisha vikosi vyake nyuma Ukraine.


Katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg ameisihi Russia kurudisha nyuma vikosi vyake.
Katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg ameisihi Russia kurudisha nyuma vikosi vyake.

Katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg, amesema Russia imeanzisha mpango wa kujiimarisha zaidi kijeshi katika mpaka wake na Ukraine na ndani ya Ukraine, kwa kupeleka vikosi, vifaa vya kisasa pamoja na mifumo ya ulinzi wa anga.

Akizungumza mjini Brussels, Jumanne, Stoltenberg ameisihi Moscow kurudisha nyuma vikosi vyake na kuchangia kupatikana kwa amani huko Ukraine ambapo waasi wanaoiunga mkono Russia wamekuwa wakipigana na majeshi ya Ukraine upande wa mashariki.

Jeshi la Ukraine limesema Jumanne kwamba mpaka sasa takriban wanajeshi watano wamekufa katika mapigano ya toka jumapili.

Moscow imeendelea kukataa kutoa msaada wa moja kwa moja kwa waasi wa Ukraine na imesema vikosi vya Russia vinavyopigana pamoja na waasi dhidi ya Ukraine ni vya kujitolea.

XS
SM
MD
LG