Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 17:39

Ufaransa yathibitisha raia wake kuhusika na mauwaji ya Kissig


Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa Bernard Cazeneuve, amesthibitisha mfaransa yupo kwenye mkanda wa video wa ISIS.
Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa Bernard Cazeneuve, amesthibitisha mfaransa yupo kwenye mkanda wa video wa ISIS.

Ufaransa imeeleza kwamba raia wake ni mmoja wa wanamgambo wanaojiita Islamic State waliopo kwenye mkanda wa video wakitangaza kuuwawa kwa mmarekani, ambaye alikuwa ni mfanyakazi wa msaada Abdul-Rahman Kassig.

Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa Bernard Cazeneuve, alimtambua mfaransa huyo Jumatatu kuwa ni Maxime Hauchard, mwenye umri wa miaka 23, ambaye likwenda Syria, zaidi ya mwaka mmoja uliopita baada ya kukaa Mauritania.

Maafisa wanaendelea kuchunguza kama mfaransa mwingine ni mmoja wa wanajihadi ndani ya mkanda wa video, unaonyesha Kassig, akiwa ameuwawa pamoja na karibu askari 18 wa Sryia.

Shirika la Syrian Obsevatory for Human Rights la Uingereza limesema kundi la Islamic State limesha waua watu zaidi ya 1,400 nchini Syria toka mwisho wa mwezi Juni.

XS
SM
MD
LG