Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 22:12

Obama athibitisha kifo cha Mmarekani aliyechinjwa na ISIS.


Ed na Paula Kassig, wakisali katika ibada ya kumwombea mtoto wao Abdul-Rahman Kassig katika chuo kikuu cha Butler huko Indianapolis, Indiana, on Oct. 8, 2014.

Rais wa Marekani Barack Obama amethibitisha kifo cha raia wa Maekani aliyekuwa ametekwa nyara Abdul Rahman Kassig akisema mfanyakazi huyo wa huduma za dharura aliuwawa katika kitendo cha ukatili mtupu na kundi la Islamic State.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari akiwa kwenye ndege ya Air Force One, akirudi nyumbani kutoka kwenye mkutano wa G 20 huko Australia Bw.Obama aliwapa pole wazazi na familia ya Kassig.

Aliwashutumu kundi la ISIS kwa kuonyesha vitendo vya kuchinja watu wasio na hatia ikiwa ni pamoja na waislam akisema inapelekea tu kwenye kifo na uharibifu.

XS
SM
MD
LG