Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 07:03

Rais Obama akutana na Aung San Suu Kyi huko Myanmar


Rais Barack Obama wa Marekani akisalimiana na Rais Thein Sein wa Myanmar kabla ya kufunguliwa mkutano wa viongozi wa ASEAN.
Rais Barack Obama wa Marekani akisalimiana na Rais Thein Sein wa Myanmar kabla ya kufunguliwa mkutano wa viongozi wa ASEAN.

Rais Barack Obama wa Marekani amekuwa na mazungumzo na kiongozi wa upinzani wa Myanmar Aung San Suu Kyi, nyumbani kwake mjini Yangon Ijuma asubuhi.

Katika mkutano wa pamoja na waandishi habari baada ya mazungumzo yao, Rais Obama alirudia wito wake wa kuwataka viongozi wa Myanmar kuendelea na kuimarisha mageuzi ya kidemokrasia nchini humo.

Bi, Suu Kyi amesema utaratibu wa mageuzi umekuwa ukikwama mara kwa mara, hata hiyo yeye pamoja na Rais Obama walieleza matumaini kwamba mageuzi yatafanyika nchini humo.

Siku ya Alhamisi Rais Obama alieleza imani yake juu ya kile alichokieleza ni "siku mpya yajitokeza" Myanmar, lakini alionya kwamba kuna kazi nyingi inahitajika kukamilisha mpito kutoka miongo kadhaa ya utawala wa kimabavu wa kijeshi kuelekea demokrasia kamili.

Rais Obama alikua na mazungumzo ya faragha na Rais Thein Sein wa Mnyanmar, wakati wa ziara yake nchini humo alipohudhuria mkutano wa pili wa viongozi wa Jumuia ya mataifa 10 ya Kusini Mashariki ya Asia ASEAN na Marekani.

XS
SM
MD
LG