Rais barack Obama wa Marekani anasema anataka kufikisha uhusiano na china katika kiwango kipya cha juu. Wakati wa siku ya kwanza ya ziara yake rasmi ya siku mbili ya mikutano mjini Bejing na Kiongozi mwenzake Xi Jinping , kiongozi huyo wa Marekani alialikwa katika dhifa rasmi Jumatatu na alisema “wakati Marekani na China zinaweza kufanya kazi pamoja kwa dhati , dunia nzima inafaidika” .
Mikutano ya Obama na Xi inafanyikia kando ya mkutano wa viongozi wa jumuia ya uchumi ya nchi za Asia na Pacifc uIiodhaminiwa na serikali ya Bejing. Mkutano ambao viongozi walitoa idhini yao ya awali ya kubuniwa kanda ya biashara huru itakayoongozwa na China.
Kutolewa idhini hiyo inachukuliwa kama mafanikio kwa Bejing ambayo imekuwa ikishinikiza kuwepo na eneo la biashara huru ya nchi za Asia na Pacifik FTAAP badala ya pendekezo jingine la kubuniwa eneo hilo litakaloongozwa na Marekani.