Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 17:41

Mauwaji ya kiholela Mombasa yazusha wasi wasi na ghasia


Kenya polisi washika zamu mbele ya Msiti Musa, mtaa wa Majeng, Mombasa
Kenya polisi washika zamu mbele ya Msiti Musa, mtaa wa Majeng, Mombasa

Ghasia zilizuka Jumapili katika mtaa wa Majengo mji wa pwani wa Kenya wa Mombasa, wakati wa maziko ya Hassan Guti aliyeuwawa siku ya Jumamosi na watu wasojulikana.

Waandamanaji walipora maduka na kuwarushia mawe polisi wakilalamika dhidi ya kuuliwa kwa kijana huyo, aliyetajwa na maafisa wa usalama kuwa ni 'jambnazi wa hatari'.

Mtu mmoja aliuliwa na wengine 20 kujeruhiwa katika ghasia za Jumapili. Polisi wanakanusha kuhusika na mauwaji ya Bw. Guti.

Mwandishi wa Sauti ya Amerika mjini Mombasa Josphate Kioko anaripoti kwamba, Bw. Guti, anatuhumiwa na baadhi ya maafisa wa usalama kuwa alikua gaidi na kuna dhana alihusika na mauwaji ya ofisa wa polisi mwezi wa Ogusti.

Baadhi ya wakazi walozungumza na Sauti ya Amerika wanasema, hali ni ya wasi wasi katika mtaa wa Majengo ambako kuna majambazi wengi wanaowaibia raia, na vijana wasio na kazi wanazusha ghasia katika mji huo.

Kuna wengine wanaodhani kuna viongozi wa kidini wanaohubiri mawaidha ya siasa kali jambo linalowasababisha vijana kusababisha vurugu.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:57 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Viongozi wa dini wanakanusha kwamba mawaidha yao ndiyo yanayochochea ghasia, bali wanasema hali ya usalama imezorota katika jiji hilo la pili kwa ukubwa Kenya.

Mnamo mwaka huu kuna idadi ya wahubiri wa dini ya kislamu walouliwa na watu wasojulikana, na hadi hii leo hakuna aliyekamatwa wala kushtakiwa kwa mauwaji hayo.

XS
SM
MD
LG