Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Machi 26, 2023 Local time: 05:04

Kikwete aendelea vyema baada ya upasuaji wa tezi dume


Rais Jakaya Kikwete atembelewa na Balozi Mulamula hospitalini

Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania anaendelea vizuri katika hopital maarufu ya John Hopkins mjini Baltimore, jimbo la Maryland baada ya kufanyiwa upasuaji wa tezi dume-prostate.

Kufuatana na maafisa walofuatana na Rais Kikwete hapa Marekani ni kwamba madaktari walomfanyia uchunguzi walipendekeza afanyiwe upasuaji huo ulofanyika bila ya matatizo.

Akizungumza na Sauti ya Amerika Katibu wa Rais wa Tanzania Prosper Mbena amesema "hali ya rais inaendelea vizuri na hatuwezi kujuwa atabaki kwa muda gani itategemea ushauri wa madaktari wake."

please wait

No media source currently available

0:00 0:01:02 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Kiongozi huyo kwa wakati huu anapumzika katika chumba chake cha hospitali iliyoko karibu km 50 kutoka mji mkuu wa Washington, na maafisa wa hospitali wanaeleza kwamba alianza kutembea kidogo leo asubuhi na jioni. .

XS
SM
MD
LG