Jeshi la Burkina Faso ambalo lilichukua madaraka Ijumaa, limetangaza kwamba litaunda serikali ya umoja wa kitaifa ili kusimamia kipindi cha mpito kilichosababishwa na kuondolewa kwa rais wa muda mrefu Blaise Compaore .
Taarifa fupi iliyotolewa jana usiku imeeleza kwamba kila kitu cha serikali ya mpito kitaidhinishwa kwa maridhiano ya pamoja lakini haikutoa maelezo ya jinsi gani itafanyika.
Tangazo la Jumapili huko Ouagadougou limefuatia saa kadhaa za mkanganyiko wa nani ataongoza taifa hilo maskini la watu milioni 17.
Muda mfupi baada ya kujiuzulu Bw.Compaore kwa lazima, wakuu wawili wa jeshi walijitokeza ni kila mmoja alidai kuwa ni kiongozi mpya. Na hapo tena Jumamosi, jeshi lilimtaja mmoja wao Luteni kanali Yakuba Isaac Zida kuwa ataiongoza serikali ya mpito, lakini upinzani umepinga.