Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 14:15

Ban Ki-moon anataka hatua zichukuliwe kuzuia ukame Somalia


Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon anataka hatua zichukuliwe kuzuia ukame mwingine nchini Somalia ambako anasema zaidi ya watu milioni tatu wanahitaji msaada wa kibinadamu.

Bwana Ban alizungumza Jumatano katika ziara yake ya muda mfupi katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu kama sehemu ya ziara yake ya mataifa kadhaa huko pembe ya Afrika.

Katibu mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa alisema Somalia inafanya maendeleo katika kuelekea kwenye uthabiti wa kisiasa lakini amesema ana wasi wasi mkubwa wa hali ya kibinadamu nchini humo na kuwataka wafadhili kuongeza michango yao.

Bwana Ban anafuatana na viongozi wa Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya nchi za Ki-Islamu na taasisi nyingine ambazo wiki hii zimeahidi takriban msaada wa dola bilioni nane kwa nchi za pembe ya Afrika.

XS
SM
MD
LG