Upatikanaji viungo

Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 22:19

Mapigano bado yanaendelea kaskazini mwa Syria.


Moshi ukiwa unafuka kufuatia shambulizi la bomu huko Kobani.
Moshi ukiwa unafuka kufuatia shambulizi la bomu huko Kobani.

Mapigano bado yanaendelea kaskazini mwa Syria kwenye mji wa Kobani kukiwa na sauti za milio ya risasi na ndege angani zikionyesha kuendelea juhudi za kuwazuia wanamgambo wa Islamic state kuchukua eneo hilo kutoka kwa vikosi vya Kikurdi.

Kamera zilizowekwa upande wa pili wa mpaka wa Uturuki zilipiga picha kile kinachoonekana kuwa mashambulizi mapya yanayoongozwa na Marekani yakilenga wanamgambo wa Islamic state nchini Syria kwa zaidi ya mwezi mmoja.

Video imejumuisha sauti ya ndege iliyokuwa inaruka na mashambulizi makubwa ya mlipuko ambayo yalisababisha moshi angani. Wapiganaji wa Kikurdi wanatarajia kuwasili kwa vikosi vya Peshmerga kutoka eneo la Kurdi la Iraq ambavyo vinategemewa kujiunga na mapambano dhidi ya wanamgambo hao huko Kobani wiki hii.

XS
SM
MD
LG