Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 05, 2022 Local time: 03:12

Mtu wa nne Marekani kuambukizwa Ebola atibiwa New York.


Watu wakipita kuingia kwenye hopitali ya Bellevue huko New York ambako Dr.Spencer anatibiwa Ebola. Oct. 24, 2014.

Daktari wa new York ambaye amekuwa akiwahudumia wagonjwa wa Ebola nchini Guinea amekuwa wa mtu wa kwanza kupatikana na ugonjwa wa Ebola katika mji huo.

Mayor wa mji Bill de Blasio alithibitisha jana huku akisema kwamba daktari Craig Spencer ametengwa na hakuna haja ya kuwa na wasi wasi.

Spencer siku ya alhamisi alilijulisha shirika la hisani la madaktari wasio na mipaka ambako alikuwa akifanya kazi kwamba ana homa kali na alikuwa akijisikia kichefuchefu ikiwa ni dalili mbili za Ebola.

Maafisa wanatafuta yeyote ambaye huenda alikuwa na mawasiliano na Spencer, ambaye amekuwa mtu wa nne kugundulika na Ebola katika ardhi ya Marekani na wa kwanza huko New York .

XS
SM
MD
LG