Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 05, 2023 Local time: 04:07

Burkina Faso yajaribu kuondoa mihula miwili ya urais .


Rais wa Burkina Faso Blaise Compaore alipokutana na na aliyekuwa mgombea urais wa Guinea 2010 Cellou Dalein Diallo huko Conakry Guinea.

Serikali ya Burkina Faso inafanya msukumo mpya kuondoa masharti ya mihula miwili ya urais wa nchi hiyo.

Waziri wa mambo ya ndani alisema Jumanne serikali itawasilisha muswaada bungeni kuitisha kura ya maoni juu ya suala hilo.

Wafuasi wa rais wa muda mrefu Blaise Compaore wametaka mabadiliko hayo ambayo yatamruhusu kugombea tena mwaka ujao wakati muhula wake wa pili utakapomalizika.

Kiongozi wa upinzani Benewende Stanislaus Sankara amesema upinzani utapinga mapendekezo ya kura hiyo ya maoni.

Amesema serikali ina agenda ya siri katika majaribio ya hivi karibuni ya mazungumzo na kwamba wana ushahidi kuwa wale walioko madarakani wanataka kuichezea katiba.” Alisema wanasubiri kuona ikiwa bunge litazingatia matakwa ya wengi au matakwa ya mtu mmoja.

XS
SM
MD
LG