Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 29, 2023 Local time: 19:16

Mapigano mapya yazuka Nigeria.


Wanajeshi wa Cameroon wakipelekwa kusaidia kupambana na kundi la Boko Haram. June 17, 2014.
Wanajeshi wa Cameroon wakipelekwa kusaidia kupambana na kundi la Boko Haram. June 17, 2014.

Mapigano mapya kati ya jeshi la Nigeria na wanamgambo wa Boko haram yanaripotiwa huko kaskazini mashariki mwa Nigeria siku chache baada ya serikali kusema pande hizo mbili zimekubaliana kusitisha mapigano.

Afisa wa jeshi na mwanachama wa kundi la kiraia la wanamgambo wameiambia sauti ya Amerika kwamba waasi walishambulia mji wa Damboa jumapili usiku. Afisa wa juu wa jimbo anasema wanajeshi hao walizima shambulizi hilo na kuuwa waasi 25.

Tukio hilo na mapigano mengine makali huko katika jimbo la Borno mwishoni mwa wiki yametia wasi wasi juu ya tangazo la kusitisha mapigano lililotangazwa na maafisa wa Nigeria Ijumaa. Kiongozi mmoja tu wa boko haram ndiye aliyethibitisha makubaliano hayo na kundi hilo linaaminika kuwa na vikundi vingi.

XS
SM
MD
LG