Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 18:19

Live Talk : Kunyanyaswa Wafanaykazi wa Afrika Mashariki Arabuni


Wafanyakazi wa Ethopia juu ya basi la polisi kabla ya kurudishwa nyumbani kutoka Saudia
Wafanyakazi wa Ethopia juu ya basi la polisi kabla ya kurudishwa nyumbani kutoka Saudia

Serikali ya Kenya imesitisha kazi za kuwapeleka wafanyakazi wa nchi hiyo katika nchi za kiarabu hadi pale serikali imekamilisha uchunguzi na kuhakikisha kuna mfumo wa kulinda maslahi ya raia wake.

Waziri wa kazi wa Kenya Kazungu Kambi, katika hatua nadra amesema amechukua uwamuzi huo kufuatia kuongezeka malalamiko ya Wakenya kunyanyaswa.

please wait

No media source currently available

0:00 0:45:16 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Amesema, anasitisha pia kazi zote za mashirika yanayowaajiri watu na kuwapeleka katika nchi za kiarabu kufanya kazi. Anasema wameanza majadiliano na mataifa hayo ya kiarabu ili kuhakikisha kwamba maslahi ya wafanyakazi yanalindwa.

Katibu Mkuu wa chama cha mawakala wa kuajiri wafanyakazi Hussein Adnan, anasema uwamuzi kwa upande moja utaruhusu kuchambua mawakali wa kwlei na wale wa bandia, na utatoa nafasi kupanga utaratibu bora zaidi kufuatilia wafanyakazi wanaopelekwa kufanya kazi katika nchi hizo za Kiarabu.

XS
SM
MD
LG