Uwanja wa ndege uliopo katika mji wa New York umekuwa wa kwanza nchini Marekani kuanza kufanya program ya uchunguzi kujua uwezekano wa maambukizo ya virusi vya ebola.
Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kennedy Jumamosi umeanza kuwafanyia uchunguzi wasafiri wanaoingia kutoka nchi za Afrika zilizokumbwa na ugonjwa wa ebola Guinea, Liberia, na Sierra Leone.
Mawakala wanawachunguza wasafiri kujua kama wana homa na dalili nyingine wakitumia karakasi za maswali na vipima joto vya bila kushika.
Baada ya wiki ijayo uchunguzi utaanza kufanyika katika viwanja vya ndege vya Newark, New Jersey , Washington, D.C, Chicago , Illinois na Atlanta Georgia.
Pamoja viwanja hivyo vitano vya ndege vilipata zaidi ya asilimia 90 ya wasafiri wanaoingia Marekani kutoka nchi za Afrika zilizoathiriwa.
Ijumaa shirika la afya duniani –WHO, lilisena idadi ya vifo kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa ebola umeongezeka kufikia zaidi ya watu elfu nne.