Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 16:11

Israel yalaumiwa kufanya mashambulizi Palestina.


Wa- palestina wakiwa wamebeba mwili wa mwanachama wa Hamas aliyeuwawa na mashambulizi ya anga ya Israel.
Wa- palestina wakiwa wamebeba mwili wa mwanachama wa Hamas aliyeuwawa na mashambulizi ya anga ya Israel.

Maafisa wa Palestina wanasema mashambulizi ya anga ya Israel yameuwa watu wawili katika mfululizo wa mashambulizi ambayo pia yanajumuisha ulipuaji wa maghorofa mawili.

Mashambulizi ya mapema Jumanne yaliharibu jengo la ghorofa 15 la maofisi na jengo la nyumba za kupanga katika ukanda wa Gaza. Watu 20 walijeruhiwa.

Israel imeonya watu kuondoka katika eneo hilo, mbinu ambayo jeshi imeitumia mara nyingi kabla ya kuvamia maeneo ambayo wanasema wanamgambo wamekuwa wakifanya operesheni zao.

Msemaji wa jeshi la Israel ameripoti kutokea mashambulizi mengi ya roketi dhidi ya Israel likiwemo moja lililoingiliwa na mfumo wa kuzuiya mashambulizi ya makombora kwenye mji wa Tel Aviv.

Wakati huo huo Misri imetoa wito tena kwa Israel na Hamas kutekeleza sitisho la mapigano na kurejea tena katika mashauriano ili kumaliza mapigano yaliyozuka Julai 8.

Misri ilipendekeza kufunguliwa njia ya kukatisha Gaza ili kuruhushu ushafirishaji wa vifaa vya msaada wa kibinaadamu na vingine vya kukarabati majengo.

XS
SM
MD
LG