Rais wa Ufaransa Francois Hollande amevunja serikali yake. Waziri Mkuu Manuel Valls amewasilisha hati za kujiuzulu kwa serikali yake ya kisoshalisti Jumatatu na Bw. Hollande amekubali na kumwamuru waziri mkuu huyo kuunda serikali mpya ifikapo Jumanne.
Hatua hiyo ya kisiasa inafuatia ukosoaji wa Waziri wa Uchumi Arnaud Montebourg juu ya sera za uchumi za nchi hiyo na kuhoji juu ya hatua zilizochukuliwa kwa upande wa bajeti na mshirika wao Ujerumani.
Ufaransa iko kwenye msukumo mkali kutoka Umoja wa Ulaya juu ya kurekebisha mfumo wake wa kifedha lakini Montebourg amehoji kama kubana huko matumizi kunakoshinikizwa na umoja wa Ulaya kutakuwa na faida yeyote kwa Ufaransa.