Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 21:42

Boti yazama na kuuwa 16 ziwa Albert.


Askari wa kikosi cha wanamaji cha Polisi ya Uganda wakijaribu kuokoa watu waliokuwa wakizama katika ziwa Albert Machi 23, 2014.
Askari wa kikosi cha wanamaji cha Polisi ya Uganda wakijaribu kuokoa watu waliokuwa wakizama katika ziwa Albert Machi 23, 2014.

Watu 16 wamefariki dunia na wengine watano kunusurika katika ajali ya boti katika ziwa Albert wilaya ya Ituri mpakani mwa DRC na Uganda.

Taarifa toka Bunia zinaeleza boti hiyo ilikuwa imebeba wachungaji na waimbaji waliokuwa kwenye safari ya kanisa kuelekea kwenye kijiji kimoja .

Akizungumza na mwandishi wa VOA mkazi wa Ituri John Kabwa amesema boti hiyo iliyokuwa na abiria 21 ilikumbana na upepo mkali uliopelekea kuzama.

Mkazi huyo pia amelaumu serikali ya nchi hiyo kwa kutojali raia na hasa vyombo vya usafiri ikiwa ni vya majini au nchi kavu na kuongeza kwamba boti nyingi zinafanya kazi zikiwa na injini mbovu wakati serikali inatoza fedha tu bila kujali ubora wa vyombo hivyo vya usafiri.

XS
SM
MD
LG