Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 16:52

Mabalozi wa Baraza la Usalama waridhka na maendeleo Somalia


Ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wakutana na viongozi wa Somalia mjini Mogadishu
Ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wakutana na viongozi wa Somalia mjini Mogadishu

Wajumbe 15 wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamepongeza kazi zinazofanywa na serikali ya Somalia baada ya kuitembelea Mogadishu kwa siku moja na kukutana na Rais Hassan Sheik Mohamud na maafisa wa serikali.

Hii ni mara ya kwanza kwa wajumbe wa baraza hilo kuitembelea Somalia na wajumbe walikwenda huko kuonesha ungaji mkono wao kwa juhudi za kurudisha utulivu na ustawi nchini humo.

Ni mara ya kwanza katika historia ya Somalia kutembelewa na mabalozi 15 wa Baraza la Usalama waloongozwa na balozi wa Uingereza Mark Lyall-Grant, na balozi wa Nigeria Usman Sarki.

Wakati wa ziara yao fupi walikutana na Rais Hassan Sheik Mohamud na Waziri Mkuu Abdiweli Shiekh Ahmed, maafisa wakuu wa serikali na wabunge . Wajumbe hao walikutana pia na maafisa wakuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa Somalia UNSOM na wale wa Umoja wa Afrika Amisom.

Wakizungumza na waandishi habari kwenye uwanja wa kimataifa wa Mogadishu balozi Grant wa Uingereza amesema wameridhika na ziara yao.

"Wajumbe wa Baraza la Usalama la umoja wa mataifa wamefika hapa kusisistiza dhamira ya dhati ya Jumuia ya kimataifa kwa maendeleo, amani na ustawi wa Somalia na kufahamu vyema changamoto zinaozikabili nchi hii," amesema balozi Grant

Rais wa Somalai Shiekh Mohamud alisema, walizungumza juu ya manedeleo yaliyopatikana na serikali yake. Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Somalia Abdirahman Beyle Duale ameiambia sauti ya Amerika kwamba,

"Kwa hakika ilikua ni siku muhimu kwetu sisi Somalia na ni ushiahidi kwamba jumuia ya kimataifa inatambua Somalia inasonga mbele. Na tunadhamira ya dhati kuhakikisha kwamba ahadi zote zilziotolewa zinatekelezwa katika kutayarisha mabadiliko ya kisiasa na kufanyika kwa uchaguzi."

Ziara hiyo inafanyika wakati muhimu kwa Somalia, pale inajitayarisha kuanzisha awamu nyingine ya mashambulizi ya kijeshi dhidi ya wanamgambo wa al-Shabab, pamoja na kukabiliana na mzozo wa kibinadamu kutokana na ukame unayotishia kuharibu maendeleo yaliyopatikana, pamoja na kuendelea na mageuzi ya kisiasa.

Mabalozi hao wa Umoja wa Mataifa wamewahimiza viongozi wa Somalia kuunda kwa haraka iwezekanavyo tume huru ya uchaguzi, kuongoza utaratibu wa kutafakari upya katiba na kuitisha kura ya maoni itakayo idhinisha katiba mwishoni mwa mwaka ujao, na kuitisha uchaguzi mkuu hapo 2016.

Wachambuzi wanasema changamoto kuu inayoikabili serikali ya Mogadishu ni utekelezaji wa mfumo wa utawala wa shirikisho, jambo ambalo tayari limezusha mivutano wiki hii kati ya viongozi mbali mbali. Serikali ya jimbo lenye madaraka ya ndani ya Puntland ilitangaza wiki hii kwamba inazuia ushirikiano wote na serikali kuu ya Mogadishu juu ya kuunda utawala wa majimbo ya kati.

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa huko Somalia Nick Kay, amewambia viongozi wa Somalia wakati ya mazungumzo ya Jumatanio kwamba ni bora kutekeleza mageuzi hayo haraka kuliko kusubiri, na Umoja wa Mataifa uko tayari kuwasaidia wasomali kutekeleza mageuzi hayo.

"Tunapongeza maendeleo yaliyopatikana, lakini tunafahamu ni utaratibu mgumu wa kisiasa kutekeleza mabadiliko ya mfumo wa shirikisho, na itahitaji juhudi zaidi hasa kuwahusisha kila mtu katika utaratibu huo," amesema balozi Kay.

Bw Kay anasema ni maendeleo mazuri wanaoshuhudia hadi hivi sasa na wako tayari kusaidia Somalia hadi mafanikio kupatikana.

XS
SM
MD
LG