Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 23, 2024 Local time: 03:45

Obama: Marekani haitobururwa katika vita vingine Irak


Moshi ukionekana hewani baada ya shambulizi la Marekani dhidi ya vituo vya wanamgambo wa Isamic State karibu na Khazer kaskazini mwa Irak
Moshi ukionekana hewani baada ya shambulizi la Marekani dhidi ya vituo vya wanamgambo wa Isamic State karibu na Khazer kaskazini mwa Irak

Rais Barack Obama amesema hatoruhusu kundi la wanamgambo wa kislamu huko Irak kuunda taifa la kando Irak ili kuweza kuwa na hifadhi ya salama kwa ajili ya ugaidi.

Akizungumza na waandishi habari Jumamosi, kiongozi huyo wa Marekani amesema "sidhani tutaweza kutanzua mzozo huo mnamo muda wa wiki chache, itabidi wa Irak wenyewe watafute suluhisho kwa mzozo wao, wakiwa na utawala wa umoja wa Irak."

Wanajeshi wa marekani watayarisha chakula cha kudondoshwa Irak
Wanajeshi wa marekani watayarisha chakula cha kudondoshwa Irak

Ndege za kijeshi za Marekani zilifanya mashambulizi mawili dhidi ya vituo vya kundi la Islamic State huko kaskazini magharibi ya Irak, siku ya Ijuma na kuharibu silaha na vifaa vyao.

Wakati huo huo ndege za kijeshi zimedondosha chakula nja mahitaji ya dharura siku ya Jumamosi kwenye mlima Sinjar, ambako maelfu ya wa Iraki wamekimbilia kufuatia mashambulizi ya wanamgambo wa Islamic State.

Rais Obama amesema aliamua kuchukua hatua hizo huko Irak kwa sababu Marekani haiwezi kukaa kimya wakati raia wasio na hatia wanakabiliwa na mauwaji, lakini haitioruhusu marekani kubururwa tena katika vita vya nchi kavu nchini humo.

XS
SM
MD
LG