Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 11, 2023 Local time: 04:49

Viongozi wa Afrika waondoka Washington wakiwa wameridhika


baadhi ya viongozi wa Afrika walohudhuria mkutano wa kihistoria na Rais wa Marekani Barack Obama.

Viongozi kutoka mataifa 50 ya Afrika waliohudhuria mkutano wa kwanza kati ya Marekani na Afrikia wanaondoka Washington kukiwa na ahadi ya dola bilioni 37 iliyotolewa na marekani.

Miongoni mwa miradi itakayo gharimiwa na fedha hizo ni mpango wa miaka mitatu hadi mitano ya usalama ambapo Marekani imeahidi kutumia dola milioni 110 kila mwaka kuimarisha usalama kwa kusaidia kukabiliana na migogoro kama vita dhidi ya Boko Haram huko Nigeria, Al shabab nchini Somalia, pamoja na makundi ya siasa kali katika kanda ya Sahel. Msaada huo utasaidia pia kuunda kikosi cha kiafrika cha kuingilia kwa dharura katika migogoro na kulinda amani kama alivyoeleza Rais Barack Obama alipokua anaufunga mkutano huo jana.

“Tutaungana na mataifa sita ambayo yameonesha uwezo mkubwa wa kulinda amani, Ghana, Senegal, Rwanda Tanzania Ethopia na Uganda. Na tutazialika nchi nyingine zisizo za kiafrika kuungana nasi kusaidia juhudi hizi kwa sababu ni dunia nzima yenye jukumu la kulinda amani Afrika.”

Msaada huo wa kijeshi ni sehemu ya juhudi za Marekani za kupanua biashara na uwekezaji. Bara la Afrika lina mataifa 6 kati ya kumi yenye uchumi unaokuwa kwa kasi dunani. Na idadi ya wakazi wa bara hilo linatarajiwa kuongezeka kwa maradufu ifikapo 2050.

Rais wa Mauritani, mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Mohamed Azizi anasema,

“Theluthi mbili kati yao watakua vijana chini ya umri wa miaka 35. Kwa wakati mmoja ni jambo zuri lakini ni changamoto”.

Changamoto yenyewe ni kuweza kuwa na miundo mbinu mizuri, elimu na ajira. Kwa upande wa ajira kulikua na matumaini mazuri kwa wakati huu kutokana na tangazo kwamba kutakuwa na uwekezaji wa dola bilioni 33 katika miradi ya biashara ya mashirika ya binafsi na umaa kama vile Coca-Cola na IBM.

Nje ya ukumbi wa mkutano kulikua na maandamano ambapo waandamanaji walikua wanalalamika dhidi ya serikali kandamizi za Afrika ambazo zinaweza kufuja uwekeji huo wa Marekani na wanadamanaji walikua na hasira na rais Obama kwa kuwaalika viongozi wa Guine, gambia na Ethopia.

Katika uapnde wa pili wa jiji hili la Washington mke wa Rais Obama, Michelle aliungana na mke wa rais wa zamani Laura Bush na kuzungumza na wake wa marais wa Afrika, na kujadili juu ya kuwawezesha wanawake wa Afrika. Laura bush,

“Mtu mmoja aliwahi kusema, kwanini hamfanyikazi na wanawake kwani wanaume ndio wanatatizo”.

Michellle akisisitiza juu ya mabadiliko

“Inabidi kubadili mtizamo kabla ya kubadili tabia.”

Katika mkutano wao walitangaza miradi kadhaa ya kuwawezesha wanawake.

Na licha ya kwamba Afrika inakabiliwa na changamoto chungu nzima lakini, Rais Obama amesema mkutano wa Washington umeonesha ukuwaji wa uchumi barani Afrika na kwamba ni bara jipya linaloinukia na lenye ustawi.

XS
SM
MD
LG