Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 28, 2024 Local time: 14:37

Idadi ya vifo yaongezeka Libya.


Moshi ukifuka kutoka upande wa uwanja wa ndege wa Tripoli.
Moshi ukifuka kutoka upande wa uwanja wa ndege wa Tripoli.

Saa 24 za ghasia huko Libya zimesababisha vifo vya watu 61 na kuifanya idadi ya waliofariki kufikia takriban 150 katika wiki mbili za mapigano nchini humo.

Takriban watu 38 waliuwawa katika mji wa mashariki wa Benghazi wakati majeshi ya Libya yalipopambana na wanamgambo wa kiislam wenye silaha Jumamosi na Jumapili.

Wafanyakazi wa Misri walikuwa miongoni mwa watu 23 waliouawa katika makao makuu ya Libya Tripoli, ambapo mapigano makali kati ya makundi ya wanamgambo yanayopingana yameingia wiki ya tatu.

Karibu watu 100 wamefariki dunia katika mapigano yanayoendelea katika uwanja wa ndege pekee tangu mapema Julai, wakati majeshi ya serikali yakipata taabu kuzuia ongezeko la hali ya juu la ghasia tangu vita vya 2011 ambavyo vilimuondoa madarakani Moammar Gadhafi.

XS
SM
MD
LG