Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 11, 2026 Local time: 01:16

Obama: Kombora ndilo liliangusha ndege ya Malaysia huko Ukraine

Mishuma imewasha kwa ajili ya kusoma dua kwa ajili ya waahiriwa wa ndege ya Shirika la Malaysia nambari 17 katika kanisa nje ya Kuala Lumpur, Malaysia, Ijuma, Julai 18, 2014.
Mishuma imewasha kwa ajili ya kusoma dua kwa ajili ya waahiriwa wa ndege ya Shirika la Malaysia nambari 17 katika kanisa nje ya Kuala Lumpur, Malaysia, Ijuma, Julai 18, 2014.

Rais Barack Obama wa Obama anasema ushahidi unaonesha kuwa ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia iliyoanguka mashariki mwa Ukraine ilitunguliwa kwa kutumia kombora lililofyetuliwa kutoka nchi kavu kuelekea angani kutoka eneo linalodhibitiwa na waungaji mkono wa Russia wanaotaka kujitenga.

Akizungumza White House Ijumaa, Rais Barack Obama aleleza vifo vya watu 298 waliokuwemo ndani ya ndege kua ni ‘jambo la kuchukiza lisiloweza kuelezeka’. Alieleza raia mmoja wa Marekani miongoni mwa waliokufa, kufuatana na habari walizopokea hadi wakati huo.

Kiongozi wa Marekani alisema " hayo ni maafa ya kimataifa, pale ndege ya nchi ya Asia kuharibiwa juu ya anga ya Ulaya ikiwa na raia wa mataifa mbali mbali. Kwa hivyo ni lazima kufanyike uchunguzi wa kuaminika wa kimataifa."

Rais Obama, aliongezea kusma kuwa ili kufanikisha uchunguzi, Russia, kundi la waasi wanaotaka kujitenga pamoja na Ukraine lazima wasitishe mapigano mara moja. "Huu ni wakati wa kudumisha tena amani na usalama Ukraine."

Ndege ya Shirika la Malaysia MH17 ilikuwa njiani kutoka Amsterdam kuelekea Kuala Lumpa wakati shambulizi la anga lilipotokea.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Lakutana

Balozi Samantha Power (kati) akizungumza kwenye Baraza la Usalama.
Balozi Samantha Power (kati) akizungumza kwenye Baraza la Usalama.

Akizungumza kwnye kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa, Ijumaa balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Samantha Power alisema chombo cha kufyetua kombora huwenda kilikuwa katika "eneo linaloshikiliwa na waasi mashariki ya Ukraine."

Akieleza kwamba haimkiniki waasi wanauwezo wa kutumia chombo hicho bila ya msaada kutoka mtu mwenye kufahamu vyema namna ya kufyetua makombora hayo.

Wakati huo huo balozi wa Ukraine katika Umoja wa Mataifa, Yuriy Sergeyev alisema Ukraine itawasilsha ushahidi kwa baraza hilo unaoonesha jeshi la Russia lilihusika katika ajali hiyo.

Serikali ya Ukraine awali iliwashutumu waungaji mkono wa Russia wanaotaka kujitenga kwa kutengua ndege huku waasi wakilaumu majeshi ya serikali. Russia inakanusha kuhusika kaika tkio hilo.

Abiria wengi waliokuwa kwenye ndege hiyo ya aina ya Boeing 777 walikuwa wa-Holanzi na wengi walikuwa wanasayansi wanaoelekea kwenye mkutano wa kimataifa wa ukimwi nchini Australia.

Bwana Obama alisema Ijumaa kuwa Marekani iko tayari kutoa msaada wa aina yeyote ikibidi. Alisema wafanyakazi wa FBI na NTSA tayari wapo njiani kuelekea katika eneo la ajali ambako kuna mabaki ya ndege hiyo na miili ya abiria ambao haijaondolewa bado.

Matukio duniani baada ya ajali ya ndege ya Malaysia

Mwanamgambo anaeunga mkono Russia akiangalia sehemu ya mbele ya ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia Boeing 777 iliyoangushwa karibu na kijiji cha  Rozsypne, jimbo la Donetsk, Julai 18, 2014.
1/9 Mwanamgambo anaeunga mkono Russia akiangalia sehemu ya mbele ya ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia Boeing 777 iliyoangushwa karibu na kijiji cha  Rozsypne, jimbo la Donetsk, Julai 18, 2014.
Matukio mbali mbali kufuatia kutenguliwa kwa ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia huko Ukraine
Mabaki ya sehemu ya mbele ya ndege ya Shirila la Ndege la Malazia aina ya Boeing 777 iliyotenguliwa Juali 18 na kuanguka katika kijiji cha Rozsypne, jimb la Donetsk, July 18, 2014.
2/9 Mabaki ya sehemu ya mbele ya ndege ya Shirila la Ndege la Malazia aina ya Boeing 777 iliyotenguliwa Juali 18 na kuanguka katika kijiji cha Rozsypne, jimb la Donetsk, July 18, 2014.
Matukio mbali mbali kufuatia kutenguliwa kwa ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia huko Ukraine
Waandishi habari wamzunguka jamaa yake abiria mmoja wa ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia nambari MH17 iliyoanguka katika eneo lenye vita Ukraine, katika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur  Sepang, Malaysia, Julai 18, 2014.
3/9 Waandishi habari wamzunguka jamaa yake abiria mmoja wa ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia nambari MH17 iliyoanguka katika eneo lenye vita Ukraine, katika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur  Sepang, Malaysia, Julai 18, 2014.
Matukio mbali mbali kufuatia kutenguliwa kwa ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia huko Ukraine
Wachimba mgodi wa mkaa wa Ukraine wakitafuta eneo ambako ndege ya Malasia ilianguka katika kijiji cha Rozsypne, mashariki ya Ukraine Ijuma, Julai 18, 2014.
4/9 Wachimba mgodi wa mkaa wa Ukraine wakitafuta eneo ambako ndege ya Malasia ilianguka katika kijiji cha Rozsypne, mashariki ya Ukraine Ijuma, Julai 18, 2014.
Matukio mbali mbali kufuatia kutenguliwa kwa ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia huko Ukraine
Candlelight prayers are prepapred for victims of the Malaysia Airlines MH17 at a church outside Kuala Lumpur, Malaysia, July 18, 2014.
5/9 Candlelight prayers are prepapred for victims of the Malaysia Airlines MH17 at a church outside Kuala Lumpur, Malaysia, July 18, 2014.
Matukio mbali mbali kufuatia kutenguliwa kwa ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia huko Ukraine
Debris is pictured at the site of the Malaysia Airlines Boeing 777 plane crash, near the village of Grabovo, in the Donetsk region, July 18, 2014.
6/9 Debris is pictured at the site of the Malaysia Airlines Boeing 777 plane crash, near the village of Grabovo, in the Donetsk region, July 18, 2014.
Matukio mbali mbali kufuatia kutenguliwa kwa ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia huko Ukraine
Aleksandr Borodai, Waziri Kiongozi wa jimbo lililojitangazia uhuru la Jamhuri ya Watu wa Donetsk, akizungumza na waandishi habari huko Donetsk, mashaiki ya Ukraine, Julai 18, 2014.
7/9 Aleksandr Borodai, Waziri Kiongozi wa jimbo lililojitangazia uhuru la Jamhuri ya Watu wa Donetsk, akizungumza na waandishi habari huko Donetsk, mashaiki ya Ukraine, Julai 18, 2014.
Matukio mbali mbali kufuatia kutenguliwa kwa ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia huko Ukraine
Jamaa wa abiria wa nege ya Shirika la Ndege la Malaysia nambari MH17 wakiwa na huzuni walipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kuala Lumpur, huko Sepang, Malaysia, Julai 18, 2014.
8/9 Jamaa wa abiria wa nege ya Shirika la Ndege la Malaysia nambari MH17 wakiwa na huzuni walipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kuala Lumpur, huko Sepang, Malaysia, Julai 18, 2014.
Matukio mbali mbali kufuatia kutenguliwa kwa ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia huko Ukraine
Kundi la waendesha baiskeli wakiwa na Maliana Vincenzo Nibali, wakikaa kimya kwa dakika moja kuwakumbuka waathiriwa wa ndege ya Malaysia nambar MH 17, kabla ya kuanza awamu ya 13 ya mashindano yao ya baiskeli ya Tour de France, Chamrousee, Ufaransa, Julai 18, 2014.
9/9 Kundi la waendesha baiskeli wakiwa na Maliana Vincenzo Nibali, wakikaa kimya kwa dakika moja kuwakumbuka waathiriwa wa ndege ya Malaysia nambar MH 17, kabla ya kuanza awamu ya 13 ya mashindano yao ya baiskeli ya Tour de France, Chamrousee, Ufaransa, Julai 18, 2014.
Matukio mbali mbali kufuatia kutenguliwa kwa ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia huko Ukraine
Previous slide
Next slide

This item is part of
XS
SM
MD
LG