Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 13:40

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Hague atangaza kujiuzulu.


Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Bw.William Hague akizungumza na waandishi wa habari mjini London.
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Bw.William Hague akizungumza na waandishi wa habari mjini London.

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague alisema jumatatu kuwa anajiuzulu kama mwanadiplomasia wa juu baada ya miaka minne katika kazi hiyo, ikiwa ni sehemu ya mabadiliko makubwa yaliofanywa na waziri mkuu David Cameron tangu kuchaguliwa kwake 2010.

Hague aliandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba anajiuzulu na hatagombea ubunge katika uchaguzi mkuu ujao unaotarajiwa kufanyika Mei mwakani.Vyombo vya habari vya Uingereza vinasema nafasi yake huenda ikachukuliwa na Phillip Hammond waziri wa sasa wa Ulinzi.

Mkuu wao Bw.Cameron ambaye ni kiongozi wa chama cha Conservative anafanya kile kinachotarajiwa kuwa mabadiliko ya mwisho ya baraza lake la mawaziri kabla ya uchaguzi huo mkuu wa kitaifa. Anatarajiwa kutangaza majina kadhaa ya mawaziri wapya Jumanne.

XS
SM
MD
LG