Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 14:29

Sudan Kusini wanasheherekea mwaka wa tatu wa uhuru wake .


Wacheza ngoma mbali mbali wakisheherekea kwa ngoma miaka mitatu ya uhuru wa Sudan Kusini huko Juba, July 9, 2014.
Wacheza ngoma mbali mbali wakisheherekea kwa ngoma miaka mitatu ya uhuru wa Sudan Kusini huko Juba, July 9, 2014.

Sudan Kusini Jumatano inasheherekea mwaka wa tatu wa kujitenga kwake na Sudan .

Lakini baadhi wanasema kuna kidogo sana cha kusheherekea ikiwa nchi hiyo iko kati kati ya vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimesababisha watu kadhaa kupoteza makazi yao na njaa ikiwa inakuja pamoja na rushwa.

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon jumanne amewataka Salva Kiir na kiongozi muasi makamu rais wa zamani Riek Machar kutimiza yale wanayotarajiwa kufanya na watu wao kwa kuweka silaha chini na kurudi kwenye meza ya mazungumzo.

Waziri wa mambo ya nje Barnaba Marial Benjamin amesema watu wa Sudan Kusini wana mengi ya kusherekea kwa sababu wana uhuru. Alisema waasi ambao aliwataja kama wafanya fujo wamekuwa wakizuia mazungumzo yaliolenga kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe.

XS
SM
MD
LG