Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 22:23

Jill Biden akamilisha ziara DRC akisisitiza kipaumbele cha elimu kwa wasichana.


Jill Biden, mke wa makamu rais wa Marekani akisalimiana na askari mtoto wa zamani huko Bukavu, Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Julai 5, 2014.
Jill Biden, mke wa makamu rais wa Marekani akisalimiana na askari mtoto wa zamani huko Bukavu, Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Julai 5, 2014.

Jill Biden mke wa makamu rais wa Marekani Joe Biden anarudi Jumatatu kutoka kwenye ziara yake ya wiki nzima barani Afrika akisisitiza umuhimu wa elimu kwa wasichana na wanawake wanaofanya kazi serikalini.

Alimaliza ziara yake ya mataifa matatu huko Sierra ambako amempongeza rais Ernest Bai Koroma, kama mfuasi wa haki za wanawake.

Biden alisema katika tukio moja jumapili kwamba amevutiwa na nchi hiyo kushawishi wasichana kumaliza elimu ya sekondari kupitia juhudi za kuzuia mimba za wasichana wadogo na ndoa za mapema.

Alisema “ Marekani ina nia ya dhati kuhakikisha wasichana na wanawake vijana wana nyenzo wanazohitaji kufanikiwa katika jamii zao.Na ushiriki wa wanawake katika nguvu kazi na kutoa maamuzi ni muhimu na chanzo cha nguvu”.

Katika hafla hiyo pia alikuwapo jaji mkuu wa Sierra Leonne , waziri wa mambo ya nje na Khadija Sam- Sumana mke wa makamu rais Samuel Sam-Sumana.

Biden alifuatana na mkuu wa shirika la USAID Rajiv Shah na balozi wa Marekani wa masuala ya wanawake duniani Catherine Russell wakati wakiendelea kueleza juu ya faida za wanawake kuhusika katika maendeleo ya kiuchumi na kuimarisha demokrasia.

XS
SM
MD
LG